Burudani

BAADA YA KUPIGWA MPAKA KUTEMA ‘UDENDA’…DULLAH MBABE ATANGAZA KUPUMZIKA NGUMI

admin October 11, 2021 1:30 pm


Bondia Abdallah Pazi โ€˜Dullah Mbabeโ€™ ametangaza kupumzika kupanda ulingoni, ikiwa ni saa kadhaa baada ya kupoteza pambano lake dhidi ya Bondia kutoka DR Congo Tshimanga Kantompa.

Jumamosi (Oktoba 09) Dullah Mbabe alikubali kuchapika kwa Point, baada ya kuangushwa mara tatu kwa ngumi nzito cha mpinzani wake Tshimanga Kantompa, kwenye pambano lililounguruma kwenye ukumbi wa PTA jijini Dar es salaam.

Bondia huyo ambaye ni namba mbili nchini Tanzania katika uzani wa Super Middle amesema amelazimika kujipa muda wa kupumzika ili kujipanga upya.

โ€œMwakani ndio nafikiria nitarudi ulingoni, ila kwa sasa wacha nipumzike kwanza, nitulize akili, nijipange upya ili niwe na ujio mpya nitakaporejea tena ulingoni.โ€ amesema Dullah Mbabe

Pambano la Jumamosi (Oktoba 09), lilikua la pili mfululizo kwa Dullah Mbabe kupoteza, baada ya kuambulia kisago kikali kutoka kwa mpinzani wake kwa hapa Tanzania Twaha Kiduku mwishoni mwa mwezi Agosti.

BASI LA AZAM FC NDANI YA ARDHI YA DAR ES SALAAM SAKHO AZUNGUMZA KISWAHILI AKIWA NA MSHIKAJI WAKE WAWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply