KAMATI ya Mashindano ya Yanga, imebadili gia angani juu ya maamuzi ya kuweka kambi ya siku tisa jijini Arusha na sasa kambi itaendelea kuwa Avic Town, Kigamboni, Dar.
Kikosi hicho ambacho kinanolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi, kwa sasa kinaendelea na maandalizi ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC utakaochezwa Oktoba 19, mwaka huu kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea.
Awali Yanga ilipanga kwamba baada ya mchezo huo, ingeweka kambi Arusha kisha Oktoba 30 icheze mechi ya ligi dhidi ya Azam kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini humo, lakini sasa mambo yamebadilika.
Akizungumza na SOKA LA BONGO, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, alisema: “Kikosi kinaendelea na mazoezi Avic Town kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu wa ligi dhidi ya KMC, kikosi kitaondoka Jumapili asubuhi kuelekea Songea na Jumatatu kitafanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo huo.