Home Azam FC AZAM FC KAMILI KUWAAVAA WAARABU WA MISRI

AZAM FC KAMILI KUWAAVAA WAARABU WA MISRI

[the_ad id="25893"]


WAWAKILISHI wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho,Azam FC wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao ujao dhidi ya Pyramids ya Misri.

Kwa sasa ni siku nne zimebakia kabla Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina kushuka uwanjani kutimiza majukumu yao.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Oktoba 16 siku ya Jumamosi saa 9:00 alasiri ambapo mchezo huo utakuwa wa awali kabla ya ule wa pili kurudiwa nchini Misri.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo wanahitaji ushindi.

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu ujao na kila mchezaji anajua mahitaji yaliyopo hivyo ni muhimu kufanya maandalizi ili kuweza kupata ushindi,”.

SOMA NA HII  BAADA YA 'KUIBANJUA KIMOKO' NAMUNGO...MGUNDA AFUNGUKA YA MOYONI SIMBA..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here