Home news Infinix NA TIGO WAZINDUA RASMI SIMU KALI YA FUNGA MWAKA.

Infinix NA TIGO WAZINDUA RASMI SIMU KALI YA FUNGA MWAKA.

 


Habari njema kwa wapenzi wa simu za mkononi Infinix, Kampuni ya simu Infinix ikishirikiana na kampuni ya mawasiliano Tigo yazindua rasmi Infinix HOT 11 na HOT 11 play, nakutambulishwa kama matoleo ya kwanza ya series ya HOT kuja na ujumla wa sifa hizi kwa pamoja ambazo memory ya GB128 kwa Ram ya 4, mAh 6000 za battery, wigo mpana wa kioo inch 6.82 na resolution ya FHD+ yenye kuonyesha matukio, kumbukumbu kupitia simu hiyo kwa quality ya juu.

Ushirikiano kati ya Infinix na Tigo huwapa wateja zaidi – huku simu hizi mahiri za kisasa zikija na intaneti ya 78GB bila malipo kwa mwaka mzima. Afisa Uhusiano Infinix, Bi Aisha Karupa alisema “Tumeitengeneza HOT 11 play na HOT 11 tukizingatia uzoefu wa mtumiaji kwa kuipa simu betri ya kudumu na chaji kwa muda mrefu ya ujazo wa battery la mAh6000 na yenye chipset ya G37 kwa ajili ya utendaji wa kazi na uchezaji wa games”,


Aliongeza, simu zote mbili zinakamera ya qualiti ya hali ya juu, HOT 11 inakuja ikiwa na kamera ya 50MP ya lenzi tatu yenye kipenyo kikubwa zaidi cha F1.6, ikiiruhusu kupiga picha nzuri katika hali ya mazingira yoyote na Infinix HOT 11 play inaweza fanya yote kupitia Megapixel 13 za kamera ya nyuma, Infinix tunamthamini na kuwajali wateja wetu na simu hii ni kama zawadi kwenu tunadhihirisha hili kupitia bei ambayo kima chake ni kuanzia sh. 335,000 katika maduka ya Tigo”.

Meneja biashara wa Tigo, Suleiman Bushagama akizungumza wakati wa uzinduzi huo alisema, “Ushirikiano wetu na Infinix ni wa kujivunia kwa sababu unaendana vyema na maono yetu ya kuleta ulimwengu mpya wa kidijitali kwa wateja. Uzinduzi huu wa aina nyingine ya juu zaidi, simu mahiri ya bei nafuu, ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kuhakikisha kwamba kila mtu anafurahia manufaa ya maisha ya kisasa yaliyounganishwa kupitia huduma na bidhaa tunazotoa.”

SOMA NA HII  BAADA YA KUKAMILISHA USAJILI NA KUNGOJA UTAMBULISHO...MNIGERIA OKWA AANZA 'KUTIBUA TIBUA' MAMBO SIMBA...

Simu hii imeanza kupatikana rasmi katika maduka yote ya simu nchini Tanzania.