Home Ligi Kuu KISA NEMBO YA MDHAMINI WA LIGI KUU NBC…BODI LA LIGI KUZISHUSA DARAJA...

KISA NEMBO YA MDHAMINI WA LIGI KUU NBC…BODI LA LIGI KUZISHUSA DARAJA TIMU ZA LIGI KUU


MTENDAJI Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Almasi Kasongo amesema kuwa Klabu ambayo haitavaa nembo ya mdhamini NBC itashushwa daraja.

Kasongo amesema kuwa katika michezo ya mzunguko wa nne kumekuwa na baadhi ya timu zimevaa nembo hiyo huku nyingine zikishindwa kufanya hivyo kama inavyotakiwa kwa mujibu wa kanuni ya 16 (1) 7 ya Ligi Kuu Bara.

Baada ya kutokea hilo kamati imeagiza Klabu zote za NBC kuhakikisha zinavaa nembo yenye mdhamini mkuu kama ilivyoelekeza kwenye kanuni ya 16 (1.1), 16 (1.3), 16 (1.7) na 16 (1.8) ya Ligi Kuu kuhusu mdhamini.

Alieleza kuwa timu yoyote itakayoshindwa kufanya hivyo itatoza faini ya Sh3 milioni na kama makosa hayo yatakuwa yakijirudia itachukuliwa hatua kali zaidi ikiwemo kushushwa daraja.

Kasongo amesema kuwa agizo hilo linaanza kutekelezwa tangu tangazo limetoka Oktoba 27, huku akivitaka Klabu, wadau wote kwa maana ya viongozi, wachezaji na mashabiki kuzingatia kanuni hizo maana ndizo msahafu na muongozo wetu.

SOMA NA HII  MERIDIANBET NA KMC WAUNGA MKONO JITIHADA ZA HOSPITALI YA KALITA MATERNITY MADALE...