Home news PAMOJA NA KUWA NA ‘ KAMGOMO BARIDI’….YANGA KIMEELEWEKA….WACHEZAJI WAMWAGIWA MAMILIONI…SIMBA WATAJWA..

PAMOJA NA KUWA NA ‘ KAMGOMO BARIDI’….YANGA KIMEELEWEKA….WACHEZAJI WAMWAGIWA MAMILIONI…SIMBA WATAJWA..


KIMEELEWEKA! Unaweza kusema hivyo baada ya Alhamisi wiki iliyopita kutoka na taarifa kwamba mastaa wa Yanga wamepanga kufanya mgomo kushinikiza malipo yao ya bonasi, hatimaye mambo yamewekwa sawa na sasa ni full kicheko kwao.

Ishu ipo hivi; Alhamisi ya Oktoba 28, 2021, habari kubwa ilisomeka; “Kisa bonasi…Mastaa Yanga watangaza mgomo.”Baada ya habari hiyo kutoka, iliwashtua viongozi wa Yanga, fasta wakatinga

kambini na kuweka mambo sawa ili tu kuondoa sintofahamu ambayo ingeweza kuwafanya waingie kinyonge katika mchezo wa juzi Jumamosi dhidi ya Azam FC.

Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Kambi ya Yanga iliyopo Avic Town, Kigamboni, Dar, kimesema kuwa kwamba, baada ya viongozi kuona taarifa ile, iliwafanya kufika fasta kambini hapo na kuweka kikao kizito na mastaa hao wakitaka kujua ni nani aliyefichua siri hiyo.

Mtoa taarifa huyo aliongeza kwamba, katika kikao hicho, mastaa hao wa Yanga walifanyiwa msako wa kutisha ili abainike aliyevujisha taarifa hizo za ukweli na uhakika, lakini hakuna aliyepatikana.

“Ile habari ya mgomo ilileta balaa kubwa kambini, viongozi walikuja wakiwa na hasira kweli wakitaka kumjua nani aliyetoboa siri wakati haikutakiwa kutoka nje.

“Wachezaji wote walisachiwa simu zao, lakini hakuna kilichopatikana. Mwisho wa siku wakazungumza nao kirafiki na kuweka mambo sawa.

“Baada ya kikao cha kwanza kufanyika Alhamisi, Ijumaa wakaja tena kuongeza hamasa kuelekea mchezo dhidi ya Azam ambapo walitoa ahadi kama kawaida yao na kutoa ile bonasi ya mechi mbili kati ya tatu walizotakiwa kutoa.

“Bonasi iliyotoka ni ya mechi dhidi ya Geita Gold na KMC ambazo jumla ni shilingi milioni 40 kwa maana ya kila mechi bonasi ya ushindi ni shilingi milioni 20, ile ya Simba ambayo bonasi yake shilingi milioni 400, wachezaji wameahidiwa watapewa Jumatatu {leo} baada ya kumalizana na Azam.

“Baada ya kikao hicho, tabasabu pana kwa wachezaji likaibuka na wakaahidi kutofanya mgomo, huku wakipania kufanya kweli kwenye kila mechi ili kufikia malengo ya kubeba ubingwa msimu huu,” kilisema chanzo hicho.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUPATA USHINDI MKUBWA JANA....MATOLA AVUNJA UKIMYA SIMBA...AFUNGUKA MAMBO YALIVYOKUWA UWANJANI..