Home news BAADA YA KUNG’AA KWENYE MECHI ZA KIMATAIFA NA BIASHARA UNITED…REDONDO APATA SHAVU...

BAADA YA KUNG’AA KWENYE MECHI ZA KIMATAIFA NA BIASHARA UNITED…REDONDO APATA SHAVU JIPYA…

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Kim Poulsen ametaja kikosi kitakachoingia kambini juma lijalo, kwa ajili ya michezo miwili ya mwisho ya Kundi J ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia.

Taifa Stars itacheza dhidi ya DR Congo jijini Dar es salaam Novemba 11, kisha itasafiri hadi Antananarivo kupambana na kikosi cha Madagascar katika mchezo wa mwisho wa Kundi J utakaochezwa Novemba 14.

Stars Inaongoza msimamo wa kundi J kwa kufikisha alama saba sawa na Benin, huku DR Congo ikiwa na alama tano zinazoiweka nafasi ya tatu na Madagascar inashika mkia wa kundi hilo kwa kuwa na alama tatu.

Katika kikosi hiko, mbali na wengine  pia kuna ingizo jipya la mchezaji wa zamani wa Simba SC anayekipiga Biashara United , Ramadhan Chombo .


SOMA NA HII  FT: SIMBA 2-0 WYDAD.....ONANA KAMA RONALDO.....BADO POINT HIZI SIMBA AFUZU....