Home Habari za michezo KUMBE ROBERTINHO ALIKUWA ANATAFUTIWA SABABU TU

KUMBE ROBERTINHO ALIKUWA ANATAFUTIWA SABABU TU

Tetesi za Usajili Simba

Mchambuzi wa soka Yahya Njenge amesema aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ alikuwa anatafutiwa sababu ya kufukuzwa na ikapatikana baada ya kufungwa na Yanga SC.

Yahya amesema, masiha ya Robertinho yalikuwa mashakani muda mrefu.

“Maisha ya Simba na Robertinho yalikuwa mashakani, ni kama walikuwa wanatafuta wapi atadondoka wamfute kazi

“Ukiangalia aina ya timu ambayo amepoteza dhidi yao (Yanga) ni timu yenye ubora na daraja la juu, mimi naamini alikuwa anatengenezewa namna yakuondoshwa.

“Hadi tunaona leo anaondoshwa huu ni mchakato wa muda mrefu na sababu imepatikana lakini siamini kama ndio tiba ya matatizo ya Simba,” alisema Yahya.

SOMA NA HII  ZAHERA WALA HATISHIKI KABISA NA LWANDAMINA, MWENYEWE AFUNGUKA HAPA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here