Home Habari za michezo METACHA AREJEA KIKOSINI YANGA

METACHA AREJEA KIKOSINI YANGA

Kipa namba mbili wa Yanga, Metacha Boniphace Mnata amerejea ndani ya kikosi hicho mara baada ya kukaa nje kwa takribani wiki tatu kufuatia tuhuma za utovu wa nidhamu.

Metacha ameonekana mazoezini Avic Town kwa mara ya kwanza tangu atoke kwenye kikosi cha timu ya Taifa kilichoitwa kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Sudan, mnamo Oktoba 15, ambapo baada ya hapo Kocha wa Yanga Miguel Gamondi alimsimsmisha Metacha kwa kushindwa kurejea kambini kwa wakati.

Kikosi cha Yanga Sc, kimefanya Mazoezi yao ya Mwisho jana kuelekea Mchezo wa leo dhidi ya Wagosi wa Kaya Coastal Union utakaopigwa majira ya Saa 12:30 Jioni katika dimba la Mkwakwani Jijini Tanga.

Metacha atarajiwa kuanza kwenye kikosi cha leo cha Gamondi kutokana na kipa namba moja, Djigui Diarra

SOMA NA HII  SPIKA WA BUNGE AMWAGA MAMILIONI...TIMU HII YAPOKEA MAPENE HAYO