Home news KUMBE!MANARA NA MORRISON WALIKIAMSHA TENA KISA MO

KUMBE!MANARA NA MORRISON WALIKIAMSHA TENA KISA MO


ALIYEWAHI kuwa Ofisa Habari wa Simba, Haji 
Manara, ambaye kwa sasa ni msemaji wa Yanga, amemtaka kiungo wa Simba, Bernard Morrison amjibu kuhusu suala la Mohamed Dewji kujiuzulu nafasi ya uenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi.

Manara amemtaka Morrison amjibu baada ya mchezaji huyo kuwa na tabia ya kujibu kwenye mtandao wa Instagram wa Manara.

Manara ameibua hoja hiyo baada ya bilionea Mo Dewji kujiuzulu kwenye nafasi yake ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba na kubaki kama muwekezaji.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara amemuuliza hivi Bernard Morrison; “Bernard nimemisi kuona ukinijibu kwenye akaunti yangu, hebu niambie kipi kimemfanya Muhamedi kujiuzulu au ni zile bilioni mbili wanazomuuliza aliziweka kwenye akaunti gani ya benki ndio maana kajiuzulu maana hapendi kuulizwa.”

Morrison naye akamjibu hivi Manara;“Kuna msitari kwenye Biblia unasema kuwa nabii huwa haheshimiki kwao, kwa hiyo sijashtuka kuona unahangaika kuzidi kuipaka matope heshima ya Mohamedi

“Tafuta kampuni yoyote ya kwako au hata mwambie Injinia Hersi Said akusaidie angalau uwe na kampuni maeneo ya Mikocheni ili walau ukae kwenye levo za Mohamedi, natamani kucheka ila imoji hazitembei.”

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU