Home news SIMBA WANAHESABU NDEFU KIMATAIFA

SIMBA WANAHESABU NDEFU KIMATAIFA


 SIMBA imetamba kuanza maandalizi ya awali ya 
mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika, unaotarajiwa kupigwa Oktoba 15, mwaka huu dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Katika Ligi ya Mabingwa Afrika Simba wamepangwa kuanzia ugenini dhidi ya Jwaneng Galaxy, inayoshiriki Ligi Kuu nchini Botswana katika mchezo wa hatua ya kwanza ya michuano hiyo.

Wabotswana hao walianzia hatua ya awali ambapo walifanikiwa kuiondosha Zilimadjou kutokea Visiwa vya Comoro kwa jumla ya ushindi wa mabao 5-1.

Baada ya matokeo ya sare katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United Jumanne iliyopita, Simba Ijumaa walisepa na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wao wa pili dhidi ya Dodoma Jiji kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu alisema: β€œTayari mpaka sasa tupo sawa. Mipango yetu ni kuhakikisha tunapambana kufanya vizuri zaidi na kutetea ubingwa wetu.

β€œLakini mbele yetu kuna majukumu ya michezo ya kimataifa ambapo tunatarajia kuwa na mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika Oktoba 15, mwaka huu ugenini dhidi ya Janweng Galaxy nchini Botswana, ambao ni lazima tuhakikishe tunapata matokeo mazuri ili kujihakikishia nafasi ya kufikia malengo ya angalau nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika tuliyojiwekea.”


SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA PHIRI....MBRAZILI ASIKIA KILIO CHA MASHABIKI SIMBA...AMUITA 'CHOBINGO' KUMPANGA..