Home Uncategorized DAVID SILVA APIGA HESABU ZA KUSEPA NDANI YA MANCHESTER CITY

DAVID SILVA APIGA HESABU ZA KUSEPA NDANI YA MANCHESTER CITY


DAVID Silva nyota wa kikosi cha Manchester City ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe la Ligi Kuu England hatakuepo ndani ya timu hiyo msimu ujao wa 2020/21.

Kiungo huyo mwenye miaka 34 aliibukia City akitokea ndani ya Klabu ya Valencia ya Hispania ambapo inaelezwa kuwa anaweza kurejea kwenye timu yake hiyo ya zamani.

Silva mwenyewe amesema kuwa hana mpango wa kuendelea kubaki ndani ya kosi hilo la City msimu ujao pale mkataba wake ambao unameguka mwishoni mwa msimu huu.

Inaelezwa kuwa City ilitumia nguvu kubwa kumbebeleza nyota huyo abaki ndani ya kosi hilo ila aligoma kufanya hivyo kwa kuamini kuwa muda wake wa kufanya hivyo umefika.

SOMA NA HII  COASTAL UNION KAMILI GADO KUREJEA KWA LIGI KUU BARA