Home Habari za michezo KISA SARE NA ALGERIA JUZI……TAIFA STARS YAPAAA FIFA…

KISA SARE NA ALGERIA JUZI……TAIFA STARS YAPAAA FIFA…

Taifa Stars

Tanzania imepanda kwa nafasi mbili katika viwango vya ubora wa Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kwa mwezi Septemba.

Ushindi wa bao 1-0 nyumbani dhidi ya Niger na sare tasa ya ugenini dhidi ya Algeria katika mechi za kuwania kufuzu fainali za Afcon 2023 zitakazofanyika mwakani huko Ivory ni matokeo yaliyoonekana kuchangia kuibeba Tanzania katika viwango hivyo vya ubora vilivyotolewa jana, Septemba 21.

Kwa mujibu wa viwango hivyo vya ubora, Tanzania imepanda hadi nafasi ya 122 kutoka ile ya 124 ambayo ilikuwepo katika viwango vilivyopita vilivyotolewa Julai.

Licha ya kutofuzu Afcon, Uganda imepanda kwa nafasi tatu kutoka ile ya 92 iliyokuwepo awali hadi ya 89 huku ikiendelea kuongoza kwa upande wa nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) huku Kenya ikiporomoka kutoka ya 105 hadi nafasi ya 109.

Argentina imendelea kuongoza kidunia ikifuatiwa na Ufaransa, Brazil, England na Ubelgiji.

SOMA NA HII  MDOMO WA IBENGE WAENDELEA KUMTAJA TAJA MAYELE 'MTETEMESHAJI'...SAFARI HII AMTOLEA UTABIRI HUU...