Home news MSUVA ATAJA ALIYEMWAMBIA AWE ANAPIGA MASHUTI MAKALI

MSUVA ATAJA ALIYEMWAMBIA AWE ANAPIGA MASHUTI MAKALI


MPAMBANAJI Simon Msuva,  nyota aliyewatungua Benin, jana Oktoba 10 Stars ilishinda bao 1-0 na kukusanya pointi tatu muhimu amesema kuwa ni baba yake mzazi alikuwa anamwambia awe anapiga mashuti makali kama yale.

Katika kundi J, Stars ikiwa na pointi 7 imetupia mabao matano huku Benin yenye pointi 7  ipo nafasi ya pili ikiwa imetupia mabao matatu, nafasi ya tatu ipo mikononi mwa DR Congo yenye pointi tano na Madagascar ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi tatu.

Msuva alitupia bao hilo akiwa ndani ya 18 kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Benin na kuzama mazima nyavuni.

“Baba yangu mzazi alikuwa ananiambia niwe ninafanya hivyo hasa kwa kupiga mashuti ya aina ile na nimekuwa nikipenda kufanya hivyo na kazi imekuwa ikionekana.

“Ushindi ambao unapatikana ni kwa ajili ya Tanzania kwa kuwa tunafanya kazi kupambania jezi ya Tanzania, “.

SOMA NA HII  SIO AL AHLY MLETENI YEYOTE, SIMBA WATAMBA