Home news SAA CHACHE KABLA YA MECHI..KAPOMBE AIBUKA NA JAMBO SIMBA…UONGOZI WATOA TAMKO..

SAA CHACHE KABLA YA MECHI..KAPOMBE AIBUKA NA JAMBO SIMBA…UONGOZI WATOA TAMKO..


KUELEKEA mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy utakaopigwa leo Jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, Nahodha Msaidizi wa Simba, Shomari Kapombe amesema wako tayari, huku akitamba wataibuka na ushindi na kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo kwani wana uhakika wa kufanya hivyo.

Simba wanaingia kwenye mchezo wa leo wakiwa wametanguliza mguu mmoja kwenye hatua ya makundi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ugenini.

Leo wanatakiwa kupata sare au ushindi ili kumaliza kazi. Kapombe alifunguka kuwa, wachezaji wote wako tayari kwa ajili ya mchezo huo ambapo malengo yao ni kuibuka na ushindi.

“Sisi kama wachezaji tupo tayari kwa ajili ya mchezo na kupata ushindi ili tujihakikishie nafasi ya kutinga hatua ya makundi, niwaombe Watanzania na mashabiki wa Simba kwa ujumla watuamini kwani tupo tayari kwa asilimia mia moja kuipigania Simba, hivyo wajitokeze kutupa sapoti.

“Matokeo ya mchezo wa kwanza tumeachana nayo, kwa sasa tunaangalia mchezo huu ili kupata ushindi, kikubwa mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi, tunawaahidi kupambana kwa ajili ya Simba na tuweze kutimiza malengo tuliyojiwekea.”

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu, alisema: “Tunahitaji kusonga mbele, tunafahamu kuwa tukipata matokeo mazuri basi tutakwenda hatua inayofuata ya Ligi ya Mabingwa ambayo ni hatua ya makundi, hilo ni lengo la kila Mwanasimba kuona tunafika hatua hiyo na kuvuka.”

SAKHO, MUGALU NJE

Katika mchezo wa leo, Simba itawakosa Pape Ousmane Sakho na Chris Mugal kutokana na kuwa majeruhi. Wachezaji hapo pia walikosena katika mchezo wa awali uliochezwa nchini Botswana.

Katika mazoezi yaliyofanyika juzi Ijumaa, Sakho alipewa mazoezi binafsi na kushindwa kufanya mazoezi pamoja na wenzake, huku Mugalu akikosekana kabisa.Akizungumza na Spoti Xtra, Daktari wa Simba, Yassin Gembe, alisema:

“Sakho na Mugalu ni ngumu kupatikana katika mchezo unaofuata dhidi ya Jwaneng, hatujafahamu itakuwaje lakini bado hawapo kamili kwa ajili ya kucheza. Kwa ufupi wanaendelea vizuri tofauti na hapo awali, kwa sasa wapo chini ya uangalizi wa madaktari.”

SOMA NA HII  BAADA YA KIMYA KIREFU..SALUM MBONDE AIBUKA NA HAYA KUHUSU SIMBA SC