Home Uncategorized HAWA HAPA WAMESHIKILIA HATMA YA NYOTA MTIBWA SUGAR ANAYEWINDWA NA YANGA

HAWA HAPA WAMESHIKILIA HATMA YA NYOTA MTIBWA SUGAR ANAYEWINDWA NA YANGA


DICKSON Job, beki chipukizi wa Mtibwa Sugar amesema kuwa anaweza kucheza timu yoyote ndani ya Bongo kutokana na uwezo wake alionao ila kuhusu timu atakayocheza anawaachia viongozi wa Mtibwa Sugar kuamua hatma yake.

Habari zinaeleza kuwa nyota huyo ambaye alikuwa miongoni mwa kikosi kilichoinua makwapa kubeba kombe la Mapinduzi baada ya kuitungua Simba bao 1-0 yupo kwenye hesabu za Yanga na Simba.

Akizungumza na Saleh Jembe, Job amesema kuwa amekuwa aksikia habari hizo ila hawezi kuzungumzia ni wapi atakwenda.

“Unajua mimi ni mchezaji siwezi kusema ninakwenda wapi kwa sasa ilihali nipo ndani ya Mtibwa Sugar, haina maana kwamba siwezi kucheza hapana ni suala la muda tu.

“Ishu ya mimi kuondoka ndani ya Mtibwa Sugar ipo kwa viongozi wangu ambao wao wana mamlaka kuhusu mimi,” amesema.

SOMA NA HII  MAJEMBE HAYA MANNE YA KIMATAIFA YAKUBALI KUTUA YANGA MAZIMA, GSM WAWEKA NENO