Home news SAA KADHAA KABLA YA KUIVAA COSTAL…HITIMANA ATEMA CHECHE MSIMBAZI..ATOA MAAGIZO MAZITO…

SAA KADHAA KABLA YA KUIVAA COSTAL…HITIMANA ATEMA CHECHE MSIMBAZI..ATOA MAAGIZO MAZITO…


KAIMU Kocha Mkuu wa Simba, Hitimana Thiery amesema anategemea kuona ubora wa safu yake ya kiungo ikiongezeka kwa ajili ya kutengeneza nafasi nyingi za kufunga mabao kwa washambuliaji wake katika michezo inayofauta.

Kauli ya kocha huyo imekuja wakati leo Jumapili Simba wakitarajiwa kuwa wenyeji wa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaofanyika Uwanja wa Mkapa, Dar.

Simba katika mchezo uliopita wa ligi kuu, walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania liliofungwa na kiungo wa timu hiyo, Rally Bwalya.

Akizungumza na Spoti Xtra, Hitimana alisema: “Tunahitaji kuongeza ubora haswa katika eneo letu la kiungo, tunahitaji viungo wetu waweze kutengeneza nafasi nyingi za kufunga kwenda kwa washambuliaji wetu, bado hatujakuwa bora sana katikati ya uwanja.

“Simba ni timu kubwa, malengo yetu kama timu kubwa ni kutwaa ubingwa, hivyo hatuwezi kutwaa ubingwa kama hatushindi mechi zetu na ili tuweze kushinda lazima tutengeneze nafasi nyingi iwezekanavyo haswa kupitia kwa viungo wetu wa kati.”

SOMA NA HII  MGUNDA AMPA 'MAKAVU LIVE' PHIRI KUHUSU UBINAFSI....AMTAKA AACHE KUJIFIKIRIA YEYE TU...