Home Geita Gold FC GEITA WAZIDI KUIFANYA LIGI KUU KUWA NGUMU….WAMSAJILI STAA WA ZAMANI ALIYEKIPIGA LIGI...

GEITA WAZIDI KUIFANYA LIGI KUU KUWA NGUMU….WAMSAJILI STAA WA ZAMANI ALIYEKIPIGA LIGI KUU UFARANSA NA YANGA..


Klabu ya Geita Gold FC imekamilisha usajili wa Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Burundi Saido Ntibazonkiza kwa mkataba wa miaka miwili ikiwa ni miezi mitatu tangu nyota huyo alipotemwa na Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake Mkoani Geita zinaeleza kuwa, Saido amekamilisha taratibu zote na viongozi wa timu hiyo na muda wowote kuanzia sasa atatua nchini.

“Ni kweli tumefikia makubaliano hayo baada ya mapendekezo ya benchi letu la ufundi, ni mchezaji mzuri ambaye licha tu ya umri wake ila tunaamini atatusaidia sana kwenye michuano mbalimbali hususani ile ya Kimataifa.” kilisema chanzo hicho.

Nyota huyo ameongea na viongozi ili kumtumia tiketi ya ndege ila ilishindikana hivyo kukubaliana kutumia gari akitokea kwao Burundi kisha maofisa mbalimbali wataenda hadi mpakani kumpokea kisha kujiunga na timu hiyo.

Nyota huyo alijiunga na Young Africans Oktoba 12, 2020 akitokea Klabu ya Vital’O ya nchini kwao huku akiwahi pia kuzitumikia timu mbalimbali za Kaysar Kyzylorda, Akhisar Belediye, SM Caen na Kysar.

Akiwa na Young Africans msimu uliopita alihusika kwenye mabao 10 katika Ligi Kuu Bara akifunga saba na kuchangia matatu (assisti) kwenye michezo 18 aliyocheza.

SOMA NA HII  YANGA KUSHUKA UWANJANI LEO MBELE YA JKU SC