Home Habari za michezo ACHANA NA LUIS MIQUISSONE… HUYU HAPA STAA MWINGINE ‘MWEUSI’ WA AL AHLY...

ACHANA NA LUIS MIQUISSONE… HUYU HAPA STAA MWINGINE ‘MWEUSI’ WA AL AHLY ANAYEPITIA MAISHA MAGUMU MISRI…


Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Afrika Kusini “Bafana Bafana” Percy Tau anazungumzwa kuachana na klabu ya Al Ahly ya Misri.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye alijipatia umaarufu akiwa na Mamelodi Sundowns kabla ya kuhamia Brighton, huku akiwa amepita kwenye vilabu klabu mbalimbali za Ubelgiji, anatajwa kuwa ameachana na klabu hiyo.

Tau alijiunga na Al Ahly kwa dau la dola za kimarekani milioni 1.8 akitokea Brighton, hatua iliyozua taharuki nchini Afrika Kusini ikizingatiwa kwamba alikuwa akihama kutoka Ligi Kuu ya Uingereza yenye ushindani mkubwa na kuwa na mvuto bora zaidi wa kimataifa hadi ligi ya Misri isiyo na sifa lakini pia yenye ushindani.

Aliona mafanikio katika siku zake za mwanzo chini ya ukufunzi wa Pitso Mosimane katika klabu hiyo, ambapo alishinda Ligi ya Mabingwa ya CAF na Kombe la Super Cup la CAF.

Lakini Majeraha yalipunguza ufanisi wake na kuonekana kwake uwanjani, jambo ambalo limeonekana kuwa moja ya sababu ya kutokuwa na ushawishi kikosini hapo.

Mara baada ya Mosimane kuondoka Al Ahly Juni mwaka huu, maswali yaliibuka kuhusu kubaki kwa Tau klabuni hapo na taarifa za kuondoka kwake zilithibitisha kwamba tangu mkufunzi wake aliyeifundisha Sundowns kuondoka, Tau amekuwa kwenye njia panda na Al Ahly.

Tau amefunga jumla ya magoli 8 tu kwenye michezo 31 aliyowahi kucheza akiwa na miamba hiyo ya Afrika.

SOMA NA HII  GAMONDI AWEKA WAZI MPANGO HUU KIMATAIFA YANGA