Home news IMEFICHUKAAH… KUMBE YACOUBA NDIYE MSHIKA ‘HIRIZI’ WA JESUS MOLOKO..UKWELI WA MAMBO UKO...

IMEFICHUKAAH… KUMBE YACOUBA NDIYE MSHIKA ‘HIRIZI’ WA JESUS MOLOKO..UKWELI WA MAMBO UKO HIVI….


KIUNGO mshambuliaji raia wa Burkina Faso, Yacaouba Songne ndiye anayemng’arisha winga Mkongomani Jesus Moloko. Moloko ni kati ya wachezaji wapya waliosajiliwa na timu hiyo katika kuiimarisha safu ya ushambuliaji ya Yanga.

Winga huyo amesajiliwa Yanga kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Mkongomani, Tuisila Kisinda aliyeuzwa Berkane ya Morocco.

Yacouba akicheza michezo minne ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar, KMC FC, Geita Gold na Azam FC amehusika katika mabao mawili ambayo amefunga Moloko kwa kumpigia asisti nyota huyo.

Mabao hayo amehusika Moloko katika mchezo dhidi ya Geita Gold na Azam uliochezwa juzi Jumamosi katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

Yacouba alianza msimu kwa spidi ndogo kwa kuanzia benchi katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambao alitokea benchi kuchukua nafasi ya Farid Mussa.

Mburkinabe huyo hivi sasa amejihakikishia nafasi kubwa ya kuanza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo inayofundishwa na Nasreddine Nabi. Kiungo mchezeshaji Feisal Salum ‘Fei Toto’ naye amepiga asisti mbili katika timu hiyo akicheza michezo minne ya ligi.

SOMA NA HII  BAADA YA KUSIKIA YANGA WANAPIGAGA 5G...WAARABU WAAPA KUKABA MWANZO MWISHO...