News

BAADA YA KUONA MAMBO MAZITO…NCHIMBI ATEMANA NA YANGA MAZIMA..UONGOZI WAFUNGUKA HAYA…

admin November 14, 2021 11:00 am


WAKATI kikosi cha Yanga kilikuwa visiwani Zanzibar kikiendelea na maandalizi ya Ligi, mshambuliaji wao Ditram Nchimbi amejiondoa mwenyewe kikosini.

Nchimbi alijiunga na Yanga Desemba 19 2019 ameitumikia timu hiyo miaka miwili baada ya kuona mambo yake sio mazuri ndani ya timu hiyo ameamua kujiengua mwenyewe.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa ni kweli mchezaji huyo hayupo pamoja na timu ni baada ya mkataba wake kumalizika na uongozi haujaonyesha nia ya kumuongeza mkataba.

“Mkataba wake umeshakwisha na mchezaji mwingine ambaye mkataba wake upo ukingoni ni Adeyum Saleh yeye anamalizia msimu huu sijajua kama uongozi utakuwa na mpango naye,” alisema.

Alisema Ditram ameshaaga hatakuwa miongoni mwa wachezaji wa Yanga akizungumzia maandalizi yao kwa ujumla alisema wanaenda vizuri na mipango ya kocha imeenda kama ilivyopangwa. “Kocha aliomba michezo miwili yote imechezwa wachezaji wote ameona mapungufu na uwezo wao hasa nyota ambao walikuwa nje kwa muda mrefu kama Yasin Mustafa amerudi na amepewa muda wa kucheza sasa ni yeye kuamua.”

PABLO AANZA KUKIWASHA SIMBA…AJIBU, MKUDE KAMA KAWAIDA YAO…GADIEL MICHAEL MHHH… USAJILI WA MCHEZAJI WA KICONGO WAIPONZA SIMBA…FIFA YAINGILIA KATI..UONGOZI WATOA TAMKO..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply