News

BAADA YA KUSIMAMISHWA KWA MUDA USIOJULIKANA NA AZAM…NEEMA YAMNUKIA ‘SURE BOY’..

admin November 14, 2021 2:13 pm

 


KUMEIBUKA taarifa kuwa Polisi Tanzania wapo kwenye mpango wa kuwasajili viungo wawili wa Azam FC, Mudathir Yahya na Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ ambao wamesimamishwa.

Taarifa hizo zinadai kuwa, Polisi Tanzania wanawataka nyota hao ili kuimarisha kikosi chao na kujiweka katika mazingira mazuri ya kuwania nafasi tatu za juu kwenye msimamo wa ligi mwisho wa msimu.

Chanzo hicho kililiambia gazeti la Spoti Xtra kuwa: “Upo mpango wa Azam FC kuachana na Mudathir pamoja na Sure Boy ambao wamesimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu.

Polisi Tanzania imekuwa timu ya kwanza kutuma ofa ya kuwataka nyota hao. Gazeti la Spoti Xtra lilimtafuta Makamu Mwenyekiti wa Polisi Tanzania, Robert Munis ili kujua ukweli wa taarifa hizo, ambapo alisema: “Mbona safi tu, kama mwalimu akiwataka hao wachezaji sisi kama viongozi tutawasajili.

“Hakuna timu ambayo haipendi kuwa na wachezaji wazuri kama hao, hususan Polisi Tanzania ambayo inataka kujiweka imara zaidi kwenye kuwania nafasi tatu za juu. Ila kwa sasa bado hakuna ripoti hiyo na timu inafanya vizuri.”

USAJILI WA MCHEZAJI WA KICONGO WAIPONZA SIMBA…FIFA YAINGILIA KATI..UONGOZI WATOA TAMKO.. PAMOJA MAKAMBO KUANZA KUFUNGA YANGA…MAYELE ASHINDWA KUJIZUIA…AMTUPIA DONGO HILI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply