MARA baada ya kufanikiwa kufunga bao la ushindi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya KMKM, mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele amesema ataendelea kufunga kadiri atakapopata nafasi.
Katika mchezo huo uliochezwa juzi Ijumaa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 yakifungwa na Jesus Moloko na Mayele. Awali iliifunga Mlandege 1-0 kupitia kwa Heritier Makambo.
Akizungumza hivi karibuni, Mayele alisema: โNafurahi kuona nimefunga bao muhimu na la ushindi kwa Yanga, malengo yalikuwa ni kushinda michezo yetu yote ya kirafiki, tumefanikiwa kwa hilo, tunawashukuru mashabiki wote ambao wamejitokea kutuunga mkono.
โKuhusu kufunga mabao natamani kuona kila siku nafunga, muhimu ni kutumia nafasi ambazo nitakuwa nazipata, nitajitahidi natimiza hilo kuhakikisha nafasi zote ambazo nitakuwa nazipata zinakuwa mabao.โ