news

IKIWA KESHO SIMBA INAKIPIGA NA RUVU…KAMA KAWA AJIBU ABAKISHWA DAR..PABLO AFUNGUKA HAYA…

admin November 18, 2021 12:00 pm


KIKOSI cha nyota 24 wa Simba kimeondoka Dar es Salaam jana tayari kwa mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting Ijumaa huku staa wa timu hiyo Ibrahim Ajibu akikosekana.

Simba wanatarajia kuwa wageni wa Ruvu Shooting kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza kwenye mchezo huo wanatarajia kukosa nyota wao watano.

Nyota wengine wanaotarajia kuukosa mchezo huo ni Jeremia Kisubi, Chris Mugalu, Thadeo Lwanga, Peter Banda na Patrick Mwenda.

Kwa mujibu wa kocha Pablo alisema atawakosa nyota hao kwa sababu mbalimbali na kuweka wazi kuwa kukosekana kwao hakutazuia wao kupata pointi tatu kwenye mchezo huo.

“Ajibu ni mgonjwa, Banda ajarudi tangu alipoenda timu ya Taifa, Mugalu, Lwanga wanasumbuliwa na majeruhi Mwenda na Kisubi pia wanaumwa,” alisema.

Nyota walioondoka ni makipa Aishi Manura, Beno Kakolanya, Ally Salim mabeki Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Gadiel Michael, Pascal Wawa, Joash Onyango, Kened Juma na Henock Inonga.

Wengine ni Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Sadio Kanout, Jimmyson Mwanuke, Abdulsamad Kassim, Dankan Nyoni, Erasto Nyoni, Hassan Dillunga na washambuliaji Meddie Kagere, John Bocco na Yusufu Mhilu.

KUELEKEA MECHI  DHIDI YA RUVU…..KAPOMBE AKIRI UBOVU SIMBA…ATOA AHADI MECHI YA KESHO…. KAMWAGA: SIMBA NA PABLO FRANCO; HATUA MOJA TU LAKINI HATUA KUBWA SANA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply