Home news PABLO AWATAJA MASTAA WATATU WA MAANA SIMBA…KISUBI, ABDULSWAMAD KUONDOLEWA….

PABLO AWATAJA MASTAA WATATU WA MAANA SIMBA…KISUBI, ABDULSWAMAD KUONDOLEWA….


KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco, mapema tu ameonekana kuridhishwa na viwango vya baadhi ya mastaa wa timu hiyo, huku akianza kuwataja watatu aliowaona siku ya kwanza.

Pablo raia wa Hispania, alitangazwa kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Novemba 6, mwaka huu akichukua mikoba ya Mfaransa, Didier Gomes. Baada ya kutambulishwa, akajiunga rasmi na timu hiyo, Novemba 10.

Kocha huyo ambayealianza kusimamia mazoezi ya timu hiyo Novemba 12, siku moja kabla ya hapo alishuhudia Taifa Stars kikicheza mechi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya DR Congo.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar, ulimalizika kwa DR Congo kushinda 3-0, ambapo Pablo alikuwa jukwaani, lengo ni kuwaona nyota wa Simba.

Baada ya mchezo huo, Pablo alizungumzia viwango vya wachezaji wake wa Simba akiwasifu Aishi Manula, Shomari Kapombe na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’.

“Aishi aliokoa mabao akiwa anatazamana na mpigaji, pia alipangua michomo kadhaa, ni kipa mzuri, Shomari na Mohammed nimewaona ni wazuri kwenye kukaba na kushambulia pia.

Nimefurahi kuwaona,” alisema kocha huyo ambaye alikuwa msaidizi kunako kikosi cha Real Madrid mwaka 2018.

Katika mechi hiyo, wachezaji wa Simba walioanza kikosi cha Taifa Stars ni Manula, Kapombe, Tshabalala, Kennedy Juma na Kibu Denis, huku John Bocco, Erasto Nyoni na Mzamiru Yassin wakiingia kipindi cha pili.

Mzamiru aliingia dakika ya 46 kuchukua nafasi ya Novatus Dismas, Nyoni alichukua nafasi ya Kennedy dakika ya

58, huku Bocco akiingia badala ya Kibu dakika ya 59. Kapombe alitoka dakika ya 71 kumpisha Kibwana Shomari, wakati Manula na Tshabalala wakimaliza dakika zote tisini.

Wakati Pablo akiwataja mastaa hao watatu, taarifa kutoka kwa mtu mmoja wa benchi la ufundi la Simba, zinasema kuna baadhi ya wachezaji wanaweza wasimalize msimu huu wakiwa kikosini hapo.

Hiyo ni kufuatia kocha huyo kutoridhishwa na uwezo wao baada ya kuwasimamia mazoezini kwa takribani siku sita.

“Baada ya kuangalia mechi ya kirafiki dhidi ya Cambiaso (ilichezwa Novemba 13, mwaka huu na kumalizika kwa sare ya 2-2), kocha hakufurahishwa na viwango vya baadhi ya wachezaji waliocheza mechi hiyo, hivyo kuna uwezekano mkubwa kwenye dirisha dogo wakatolewa kwa mkopo au kuuzwa kabisa,” alisema mtoa taarifa huyo.

SOMA NA HII  TETESI : KOCHA WA AL AHLY KUTUA SIMBA SC...MPANGO MZIMA UKO NAMNA HII...

Baadhi ya wachezaji wanaotajwa kuwa kwenye orodha ya hao wanaoweza kuondolewa ni Jeremiah Kisubi na Abdulswamad Kassim.