Home news BAADA YA KUUONA MZIKI WA SIMBA…KOCHA WA RED ARROWS ATIKISA KICHWA KISHA...

BAADA YA KUUONA MZIKI WA SIMBA…KOCHA WA RED ARROWS ATIKISA KICHWA KISHA AFUNGUKA HAYA..

 


Kocha Mkuu wa kikosi cha Red Arrows ya Zambia, Chisi Mbewe wamejipanga kupambana dhidi ya Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, ili kufikia lengo la kusonga mbele kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu 2021/22.

Red Arrows watacheza mchezo wa Mkondo wa kwanza dhidi ya Simba SC Jumapili (Novemba 28), Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam, kisha watamalizia nyumbani kwao Zambia kwa mchezo wa Mkondo wa pili mnamo Desemba 05.

Kocha Chisi Mbewe amesema wanafahamu wanakutana na timu ngumu ya Simba SC, na ina uzoefu wa mashindano ya kimataifa, lakini wamejipanga kupambana hadi dakika ya mwisho.

“Tunakwenda kupambana na Simba, tunatambua ubora wao na uzoefu mkubwa katika mashindano haya ya kimataifa hivyo lazima tupambane ili tuweze kuyafikia malengo yetu ambayo ni kufuzu kwenda katika hatua inayofuata ya michuano hii.”

“Kila kitu ni malengo, kama tutafanikiwa kupata matokeo mazuri katika mchezo wa kwanza tukiwa ugenini basi naamini tutaimaliza mechi vizuri tukiwa nyumbani, muhimu ni kupambania tu malengo kama ambavyo sisi tutafanya.” amesema Kocha Chisi Mbewe ambaye tayari ameshaanza safari ya kikosi chake ya kuelekea Jijini Dar es salaam.

Simba SC iliangukia kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya kutolewa kwenye Michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa kufungwa nyumbani Dar es salaam mabao 3-1 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Kabla ya mchezo huo Simba SC ilishinda ugenini mjini Gaborone mabao 2-0, hivyo Mabingwa hao wa Tanzania Bara walitupwa nje kwa kufungwa mabao mengi nyumbani.

SOMA NA HII  NEEMA ZAZIDI KUMIMINIKA YANGA....WASAINI MKATABA WA KUIPA KLABU MABILIONI YA PESA KAMA SIMBA....KAZI NDIO INAANZA...