Habari za Yanga Leo
INSHU YA MADENI YANGA…WACHEZAJI WAFUNGUKA
Abubakar
August 22, 2024
12:06 pm
Baadhi ya nyota wa zamani nchini wametoa maoni juu ya hali hiyo akiwamo kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Sekilojo Chambua amesema timu kubwa kama Yanga inachohitaji ni uchunguzi wa muda mrefu ili kuweza kufahamu mchezaji yupi anaifaa.
“Waongeze skauti kubwa ili kupunguza matukio ya kesi kama hayo, kwani sio sifa nzuri kwa klabu kama ile kuwa na sifa za namna hiyo, hata hivyo wana kikosi kipana ndio maana kabla hawajawaza kusajili wajue madhaifu yapo kwa ukubwa gani,” alisema Chambua na kuongeza:
“Kuwa na wachezaji wengi ni vizuri lakini mahitaji ndio jambo la msingi kama kuna eneo wapo wa kutosha basi haina haja ya kusajili zaidi.”
Mshambuliaji wa zamani Simba, Dua Said amesema: “Uongozi wa Yanga ujipange upya na ikiwezekana matukio haya yawe mwisho ili kuunda kikosi chenye sifa bora ndani na nje.
“Klabu kubwa inatazamwa na wengi hivyo kama itakuwa na makosa basi wapo watakaowaiga, ila jambo la msingi la kushauri ni utulivu wa hali ya juu ufanyike ili kupata kitu kilicho bora na kuchukua mchezaji ambaye alikotoka alikuwa akicheza.”