Home Habari za Yanga Leo REKODI YA YANGA CAF NA TIMU ZA ETHIOPIA

REKODI YA YANGA CAF NA TIMU ZA ETHIOPIA

CAF

KLABU ya Yanga dhidi ya timu za Ethiopia katika michuano ya CAF ina rekodi ya kuzitoa mara tatu kati ya nne walizokutana huku yenyewe ikitolewa mara mmoja hatua ya mtoano.

Yanga mbali ya kuzitoa timu hizo za Ethiopia lakini inajivunia rekodi yake ya kufunga mabao mengi wanapocheza na Wahabeshi hao.

Hata hivyo pamoja na Yanga kuzionea timu za Ethiopia bado mabingwa hao wa kihistoria Tanzania hawajawahi kushinda Ethiopia wakitoka sare mbili na kufungwa mbili wanapocheza ugenini.

Yanga ilikutana kwa mara ya kwanza klabu ya Ethiopia mwaka 1969, katika mechi ya Klabu Bingwa Afrika sasa Ligi ya Mabingwa Yanga ilitoa Saint-George ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 5-0.

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Ethiopia timu hizo zilitoka suluhu na mechi ya marudiano Yanga ilishinda 5-0 na kusonga mbele hadi robo fainali.

Kisha Yanga ilikutana na Coffee FC ya Ethiopia mwaka 1998 na kuitoa kwa jumla ya mabao 3-8, katika hatua ya mtoano wa Ligi ya Mabingwa.

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Ethiopia Coffee FC ililazimisha sare 2-2 katika mchezo wa marudiano Yanga ilishinda 1–6 nyumbani na kufanikiwa kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa.

Katika Kombe la Shirikisho mwaka 2011, Yanga ilitolewa kwa jumla ya mabao 6-4, ilianzia nyumbani na kulazimishwa sare 4-4 na Dedebit kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mchezo wa marudiano uliofanyika Ethiopia wenyeji, Dedebit walichapa Yanga mabao 2-0.

Mwaka 2018, ilicheza dhidi ya Welaita Dicha katika Kombe la Shirikisho na kufuzu hatua inayofuata kwa jumla ya mabao 2-1. Mchezo wa kwanza nyumbani Yanga ilishinda 2-0, ilipoenda ugenini ikafungwa 1-0.

LIGI YA MABINGWA

1969 Yanga 5-0 St. George

1969 St. George 0-0 Yanga

1998 Coffee FC 2-2 Yanga

1998 Yanga 6-1 Coffee

2024 CBE vs Yanga?

SHIRIKISHO

2011 Yanga 4-4 Dedebit

2011 Dedebit 2-0 Yanga

2018 Yanga 2-0 Welaita Dicha

2018 Welaita Dicha 1-0 Yanga

SOMA NA HII  BAADA YA KUSAJILIWA KWA MBWEMBWE...STRAIKA MPYA YANGA AIBUKA NA KUWEKA HADHARANI MAMBO HAYA...