Home news BAADA YA KUSAINI MKATABA..FRANKO ALETA MAFUNDI WAWILI SIMBA…FASTA AANZA NA POSHO ZA...

BAADA YA KUSAINI MKATABA..FRANKO ALETA MAFUNDI WAWILI SIMBA…FASTA AANZA NA POSHO ZA WACHEZAJI..


Tayari inafahamika kwamba kocha mpya wa Simba, Mhispania Pablo Franco Martine amesaini miaka miwili lakini akawatajia mafundi wanne.

Amewaambia viongozi anataka kocha wa makipa, wa viungo, kocha msaidizi pamoja na mtathmini wa viwango vya wachezaji.

Wakubwa wakashtuka kidogo. Wakamwambia kwa kuanzia aje na wawili – kocha wa makipa na wa viungo, ila hao wengine aangalie kwanza hawa waliopo pamoja na mazingira ya kazi.

Kocha Franco ambaye amekuwa gumzo kwa sasa mitandaoni kutokana na ukubwa wa rekodi na timu alizowahi kupita ikiwemo Real Madrid ya Hispania, ametua Tanzania leo na amewaambia Simba kama wakienda naye sambamba msimu huu klabu hiyo itafanya vizuri zaidi na waondoe hofu. Simba ilitimua wataalamu wote wa kigeni waliokuwa chini ya Didier Gomes akiwemo Adel Zrane na Milton Nienov.

Kocha huyo amewaambia viongozi wa Simba kama wakiafikiana katika mambo aliyopendekeza itamrahisia kufanya kazi yake kwa kuwapa mafanikio na kuwatoa walipo sasa.

“Atakuja na watu wawili ambao naamini watashirikiana vizuri na wengine waliopo kuiwezesha timu yetu kufanya vizuri, kama kuna ulazima tutaboresha akishafika,” alidokeza mmoja wa wajumbe ya Bodi ya Simba.

Alisema kwamba wanaamini akiona waliopo na mazingira ya kufanyia kazi atajua jinsi ya kuwatumia na viongozi wanaamini kwamba ana wasiwasi nao kwavile hajaona utendaji wao. Simba imemshauri Franco kufanya kazi kwa angalau muda wa miezi miwili na kocha msaidizi Hitimana Thiery pamoja na mtathmini wa viwango vya wachezaji, Calvin Mavunga kisha awapime kama wanafaa kuendelea kuwemo au ikishindika wawekwe kando.

MKATABA WAKE

Inafahamika kwamba miongoni mwa vipengele kwenye mkataba wa Franco ni kila mwisho wa mwezi atakuwa anachukua mshahara wa Dola 20,000 ambao kwa pesa ya kibongo ni zaidi ya Sh40 milioni.

Simba katika kumpata Franco walimpa dau nono la kumchomoa kutoka kwa waajiri wake Qadsia SC ya Kuwait ambapo walimjaza kiasi cha Dola 50,000 (Sh 100 milioni ambayo ilitumika kama ushawishi. Hiyo imeingia tu kwenye akaunti yake ili akubali kusaini mkataba.

SOMA NA HII  HAKUNA UNYONGE AL AHLY ANAPIGIKA MBONA

Kama atatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara atapewa Dola 10,000 zaidi ya Sh20 milioni ikiwa ni bonasi.

Simba wapo hatua ya mtoano kombe la Shirikisho Afrika na mkataba wa Franco unaeleza kama ataifikisha timu hiyo hatua ya makundi atapa bonasi ya Dola 5,000 ambayo ni zaidi ya Sh10 milioni.

Kwenye majadiliano ya mkataba, Franco aliwambia Simba kwa kuwa wameondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika basi bonasi, posho ambazo wamemuahidi waziweke katika Kombe la Shirikisho Afrika ili yeye na wachezaji wake wafaidi na kupata morali zaidi kama ilivyokuwa misimu miwili mfululizo kimataifa. Simba katika mkataba walikubaliana kama Franco ataifikisha timu hiyo robo fainali atapata Dola 10,000 zaidi ya Sh20 milioni kama bonasi wakati nusu fainali itakuwa Dola 15,000 zaidi ya Sh30 milioni.

Franco kama atafika tu fainali ya kombe la Shirikisho Afrika bila kujali matokeo yatakuaje watampa bonasi ya Dola 20,000 zaidi ya Sh40 milioni na akichukua ubingwa wanaweza kumpa mara mbili ya hapo.

Ikumbukwe kila timu inayotinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika, inajihakikishia kitita cha Sh 633 milioni hivyo Franco atapata 1.8% ya fedha hiyo.

Mahitaji mengine yaliyokuwa katika mkataba wa Franco ni yale ya kawaida kama kupewa nyumba nzuri yenye hadhi na tayari Simba wameshaipata ipo Ufukwe wa Bahari ya Hindi ene la Mbezi.

Franco ameandaliwa gari ya kutembelea aina ya Toyota Crown pamoja na dereva lakini kama atakuwa anatamani nyingine anaweza kubadilishiwa.

Simba watampatia tiketi mbili za ndege kwenye daraja la kwanza ‘Businnes Class’, kwa msimu mmoja kwenda na kurudi kwao Ufaransa ilipo familia yake.