Home news BAADA YA KUTUA TZ..FRANCO AIPAMBA SIMBA KWA SIFA HIZI…’ALAMBA MIAKA MIWILI’ CHAP...

BAADA YA KUTUA TZ..FRANCO AIPAMBA SIMBA KWA SIFA HIZI…’ALAMBA MIAKA MIWILI’ CHAP CHAP


KOCHA wa mpya wa Simba, Pablo Franco Martine saa 4:00 asubuhi ya leo (Jumatano), amewasili nchini kutokea Hispain kupitia Zanzibar na Shirika la ndege la Fly Dubai.

 Katika Uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, Franco aliwasili pamoja na wakala wake Mkenya kisha kupokelewa na Mratibu wa Simba, Abbas Ally kisha kumpeleka moja kwa moja katika ofisi kwao.

Franco ambaye alionekana kuwa na furaha alichukuliwa na Ally kisha kupelekwa moja kwa moja katika ofisi za Simba kwenda kuonana na Ofisa mtendaji mkuu, Barbara Gonzalez.

Kabla ya kuondoka uwanja huo wa ndege Franco amesema “Nimefurahi kuja hapa Tanzania kuifundisha timu kubwa Afrika kama Simba najisikia vizuri na tutaonana baada ya muda mfupi.”

Franco baada ya kuonana na Barbara walizungumza kisha kusaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara.

Baada ya kumaliza zoezi hilo la kusaini alikwenda kupumzika katika moja ya hoteli kisha jioni ya leo Novemba 10 atakwenda katika kambi ya Simba ambayo inaendelea na mazoezi ya nguvu katika gym.

SOMA NA HII  DILI LA MAZNOKI LAFIKIA PATAMU SIMBA....MGUNDA AKABIDHI MAJINA YA VIFAA VIPYAA...