Home news BAADA YA KUWAONA MASTAA WA SIMBA…PABLO AKUNA KICHWA ..KISHA AFUNGUKA HAYA…

BAADA YA KUWAONA MASTAA WA SIMBA…PABLO AKUNA KICHWA ..KISHA AFUNGUKA HAYA…


KOCHA mpya wa Simba, Pablo Franco amesema kuwa ni mara yake ya kwanza kufanya kazi Afrika lakini Simba mpya inakuja kwenye ubora wake.

Amesisitiza kwamba katika mkataba wake wa miaka miwili ndani ya klabu hiyo kubwa Afrika anategemea kufanya mambo makubwa na ametumia muda wake kujifunza mambo mengi ya Simba na anajua wapi pakuanzia.

Alisema jambo la kwanza ni kuhakikisha Simba inarejesha heshima yake na inakuwa imara kwenye mashindano yote matatu makubwa inayoshiriki kwa sasa Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho (ASFC) na Kombe la Shirikisho Afrika ambayo kila moja ameweka malengo yake.

“Tukichukua ubingwa wa ligi maana yake tutapata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao kwani hapo viongozi wamenieleza malengo yao ya muda mrefu katika mashindano haya wanatamani siku moja kuona wanafika mbali au kuchukua ubingwa kabisa.”

“Tupo katika kombe la Shirikisho Afrika nitatengeneza umakini mkubwa kwa wachezaji wangu kuhakikisha tunakwenda kupambana katika mechi hiyo ya mtoano,” aliongeza kocha huyo wa zamani wa Getafe.

Alisema anafahamu atakutana na ushindani wa kutosha kutoka katika maeneo tofauti ili kutimiza malengo hayo makubwa lakini amejipanga kuona yanatimia kwa ushirikiano na wasaidizi wake.

“Nitapata muda zaidi wa kuwaangalia wachezaji wote kwa pamoja kwani wengine wapo katika timu za taifa na baada ya hapo nitakuwa na kikosi imara,” alisema.

ASHUSHA MHISPANIA MWINGINE

Jana asubuhi Pablo alisimamia mazoezi ya kikosi cha Simba yaliyofanyia kwenye Uwanja wa Isamuyo kuanzia saa 2:30 mpaka saa 3:30 asubuhi.

Za ndani kabisa ni kwamba Simba walipanga kumleta aliyekuwa kocha wa viungo wa Rayo Vallecano, Mhispania aliyetambulika kwa jina moja la Miguel, ila wameshindwana masilahi.

Ila wamefikia makubaliano na kocha mwingine wa viungo ambaye ni Mhispania pia na atatua nchini muda wowote kuanzia sasa wakati unasoma hapa kuchukua nafasi ya Adel Zrane ambaye alipigwa chini.

Simba mechi ijayo wanakiwasha na Ruvu Shooting, Jijini Mwanza.

SOMA NA HII  : FURSA YA UTAJIRI NI SHINDANO LA EXPANSE KASINO NDANI YA MERIDIANBET....