Home FA Cup SIMBA KUWAPA MKWANJA WACHEZAJI WA DODOMA JIJI

SIMBA KUWAPA MKWANJA WACHEZAJI WA DODOMA JIJI


 UONGOZI wa Dodoma Jiji umeweka wazi kwamba kuelekea mchezo wa leo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba watatoa bonasi nono kwa wachezaji wake ikiwa watashinda.

Hivyo ikiwa wachezaji wa Dodoma Jiji watashinda mchezo wa leo mbele ya Simba basi watapewa mkwanja mrefu kwa ajili ya matumizi yao.

Dodoma Jiji inayonolewa na Kocha Mkuu, Mbwana Makata leo Mei 26 ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho.

Jana Mei 25 kikosi kilifanya maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa leo ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku.

Ofisa Habari wa Dodoma Jiji, Mosez Mpunga amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo na wameweka bonasi ambayo itakuwa kubwa ikiwa wachezaji watashinda.

“Kawaida huwa tunaweka bonasi kwa wachezaji pale ambapo wanashinda mechi zao na sio mchezo huu bali kila mchezo huwa tunafanya hivi kwa kuwa tunahitaji ushindi.

“Lakini kutokana na umuhimu wa mechi yetu dhidi ya Simba basi tutaongeza bonasi ili kuweza kuwapa ari wachezaji wetu waweze kupata ushindi, mashabiki wajitokeze tupo tayari,” amesema.

Mchezo wa leo nyota wao Anuary Jabir atakosekana pamoja na Rajab Mgangula kwa kuwa wanasumbuliwa ni majeruhi. 

SOMA NA HII  ORODHA YA TIMU AMBAZO ZIMETINGA HATUA YA ROBO FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO