Home Yanga SC YANGA: TUTAIPIGA SIMBA PALEPALE KWENYE MSHONO

YANGA: TUTAIPIGA SIMBA PALEPALE KWENYE MSHONO


 UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba kuelekea kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba, wataipiga kwenye mshono ambao waliwashona walipokutana Uwanja wa Mkapa.


Ikumbukwe kwamba Julai 3, Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 0-1 Yanga ulikuwa ni mchezo wa  ligi na mtupiaji alikuwa ni Zawad Mauya.

Wanakwenda kukutana kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho, Uwanja wa Lake Tanganyika ikiwa ni mchezo wa fainali, Julai 25.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz alisema kuwa wanakwenda kuwapiga wapinzani wao palepale kwenye mshono.

“Tulikutana nao Uwanja wa Mkapa bila wachezaji wenye majina tukaamua mchezo kupitia Mauya, sasa tunakwenda kuwapiga palepale kwenye mshono.

“Hamna namna sisi hatusemi sana ila tunatenda, tunajivunia mashabiki wetu ambao wapo pamoja nasi kila wakati, wadhamini wetu GSM pamoja na kazi kubwa ambayo inafanywa na Waandishi wa Habari kufikisha taarifa basi tukutane Kigoma,” alisema Nugaz.

SOMA NA HII  SAIDO ABAKIZA SIKU 40 KUENDELEA KUKIPIGA YANGA...UONGOZI WAMCHUNIA..SENZO AFUNGUKA HAYA...