Home news HITIMANA ASHINDWA KUJIZUIA… AANIKA SABABU ZA SIMBA KUTESEKA…AWATAJA CHAMA NA MIQUISSONE…

HITIMANA ASHINDWA KUJIZUIA… AANIKA SABABU ZA SIMBA KUTESEKA…AWATAJA CHAMA NA MIQUISSONE…


KOCHA Mkuu wa Simba,  Thierry Hitimana amefunguka mambo matatu yanayosababisha washindwe kufanya vizuri tangu kuanza kwa msimu huu.

Hitimana amefichua mambo hayo kufuatia Simba kucheza mechi nne katika Ligi Kuu Bara ambapo imefanikiwa kushinda mechi mbili na kutoka sare mechi mbili huku ikiwa ya katika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi kuu ikiwa pointi nane.

Leo Jumatano, Simba inatarajia kucheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo katika mchezo ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar.

Akizungumza na Championi Jumatano, Hitimana alisema kuwa, wanapitia wakati mgumu kwa sasa kutokana na timu yao kukwamishwa na uwepo wa mambo matatu ambayo hayakuwepo katika msimu uliopita hali iliyopelekea kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi Kuu.

“Tuna mambo matatu ambayo tunapitia lakini jambo la kwanza presha imekuwa kubwa ingawa ni kawaida katika soka lakini kwetu imekuwa kubwa kwa sababu tumekuwa na matokeo mabaya ambayo mashabiki wa Simba Hitimana Simba ataja… walikuwa hawajayazoea maana msimu uliopita timu ilikuwa juu sana.

“Lakini kukosekana kwa wachezaji kama Clatous Chama na Luis Miquissone wao walisaidia kwa sehemu kubwa Simba kufanya vizuri ukiangalia kwa nafasi ambazo wanacheza, Chama atacheza kumi na Miquissone 11 ambao walisaidia ila sasa wengi bado wapya hivyo shida ipo ambayo itakuwa ya mpito kwetu.

“Ukiangalia tuna wimbi kubwa la wachezaji ambao wapo majeruhi, mtu kama Chris Mugalu hayupo, Lwanga hayupo ambao hao wanaanza kwenye kikosi hali ambayo inatulazimu kuwatumia wachezaji wengi ambao wanakaa benchi na kuendelea kujipanga ili tufanye vizuri ikiwemo mechi yetu ya kesho (leoJumatano),” alisema Hitimana.

SOMA NA HII  WALICHOSEMA WACHAMBUZI WAKIFARANSA WAKATI WAKIMCHAMBUA MAYELE....ABATIZWA JINA JIPYA....