Home news HIVI NDIVYO WACHEZAJI WA KICONGO WANAVYOCHOTA PESA ZA YANGA NA GSM...

HIVI NDIVYO WACHEZAJI WA KICONGO WANAVYOCHOTA PESA ZA YANGA NA GSM KIULAINIII KABISA….

[the_ad id="25893"]


YANGA ilikuwa mkoani Lindi ikicheza na wabishi wao, Namungo na kulazimishwa sare ya 1-1 na kutibuliwa rekodi, lakini unaambiwa mastaa wao wawili wa kigeni wameshtua Jangwani kwa kuigharimu timu hiyo katika kikosi cha msimu huu.

Vinara hao wa Ligi Kuu Bara iliyolala jana kwenye Uwanja wa Ilulu, mjini Lindi, msimu huu wana mastaa kipa Diarra Djigui mabeki Djuma Shaban, Yannick Bangala kiungo Khalid Aucho, winga Jesus Moloko, washambuliaji wakiwa Heritier Makambo na Fiston Mayele.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga ni kwamba katika orodha hiyo, Mayele na Djuma ndio wachezaji walioighalimu timu hiyo fedha nyingi katika usajili wao.

Djuma na Mayele waliosajiliwa msimu huu takwimu zao zinaonyesha kuwa, wameighalimu Yanga kiasi cha Dola 100,000 (zaidi ya Sh 220 Milioni) kila mmoja katika usajili wao wakiwa ndio wachezaji ghali nchini.

Nyuma ya mastaa hao yupo Moloko aliyesajiliwa AS Vita naye ameighalimu Yanga kiasi cha Dola 90,000 (zaidi ya Sh198 Milioni) ambapo Wakongomani hao waligoma kumuachia wakiona kikosi chao kinabomolewa.

Hata hivyo kosa kubwa la Yanga lilikuwa ni kumuuza kwanza winga Tuisila Kisinda kwa klabu ya RS Berkane kisha wakatua kwa Moloko ambaye alicheza na Kisinda wakiwa hapo AS Vita.

Kwa upnde wa viungo Aucho na Bangala ubora wao wa uwanjani na kucheza pamoja hautokani hivi hivi tu, bali ni kutokana na kukunja mzigo wa maana kwenye usajili wao kwani kila mmoja amevuta Dola 55,000 (Sh121 Milioni).

Kipa Diarra naye hayupo mbali kwenye orodha hiyo kwani ameighalimu Yanga kiasi cha Dola 50,000 (Sh110 Milioni) ambapo kidogo Yanga wamkose kufuatia kuwa na ofa ya nchini Afrika Kusini lakini ikatua kwake akiwa tayari ameshasaini Yanga.

Straika anayeshikilia rekodi kwa misimu ya hivi karibuni kuifungia Yanga mabao mengi ndani ya msimu mmoja kabla ya kuuzwa Guinea, Makambo ambaye bado hajafunga bao katika mechi za mashindano ameighalimu Yanga kiasi cha Dola 45,000 (Sh 99 Milioni).

Mmoja wa watu wa karibuni kutoka ndani ya Yanga, alisema utamu unaaoonekana kwa timu yao inayosifika kwa kupiga pasi nyingi, umetokana na usajili huo wa kishindo na anaamini mwisho wa msimu utalipa tofauti na uilivyokuwa msimu minne iliyopita timu yao ikitoka kapa.

SOMA NA HII  KISA MAYELE KUKOSA PENATI JUZI...NABI NAYE KAONA LISIMPITE HIVI HIVI...AIBUKA NA HILI JIPYA...

“Yanga inayoonekana nzuri haitokani na kingine ila ni usajili mzuri wa gharama na imani ya wanayanga mambo yatajipa,” alisema kigogo huyo aliyeomba kuhifadhiwa jina.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here