Home news KIMEELEWEKA…ISHU YA YANGA KUVAA NEMBO NYEUSI YA MDHAMINI..BODI YA LIGI WAJA NA...

KIMEELEWEKA…ISHU YA YANGA KUVAA NEMBO NYEUSI YA MDHAMINI..BODI YA LIGI WAJA NA HILI…


MKURUGENZI wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo ametoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya vilabu vya soka nchini kubadili nembo za wadhamini kwenye jezi zao.“Suala la nembo ni suala la kikanuni na bodi ya ligi kazi yake kusimamia kanuni mwenye dhamana ya kusimamia hilo ni yule mwenye nembo yake.

“Bodi ya ligi inanembo yao TFF ina nembo yao na kila klabu ina nembo yake. Bodi tutasimamia kanuni zinavyosema na pia tutazingatia makubaliano baina ya mwenye nembo na klabu husika.

“Na haiwezekani mwenye nembo aseme tumekubaliana na mhusika flani halafu bodi ipinge, bodi ipo kwa ajili ya kusave interest ya klabu na bodi ya ligi ni sulihisho na si kuwa chanzo cha tatizo kwa wadau wetu,” CEO TPLB Almasi Kasongo akitolea ufafanuzi kwanini wamekubali Yanga SC kuvaa twiga mweusi.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA SIMBA NA YANGA...HUU HAPA UDHAIFU WA WATANI WA JADI