Home news KISA UVIVU WA WACHEZAJI SIMBA…PABLO AIBUKA NA JIPYA MSIMBAZI..ATOA KAULI YA KIBABE….

KISA UVIVU WA WACHEZAJI SIMBA…PABLO AIBUKA NA JIPYA MSIMBAZI..ATOA KAULI YA KIBABE….


KOCHA mkuu wa Simba, Pablo Franco ameweka wazi kuwa anataka kuona kila mchezaji wa timu hiyo anapambana kuhakikisha anafanya bidii mazoezini na kila anapopewa nafasi kwa kuwa amepanga kumpa kila mchezaji nafasi ya kucheza.

Pablo juzi Jumapili aliiongoza Simba kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam, kwa ajili ya mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows ya Zambia.

Tangu atangazwe na Simba kuwa kocha mkuu mpya wa timu hiyo, Pablo amefanikiwa kuiongoza Simba katika michezo miwili ya kimashindano rasmi dhidi ya Ruvu Shooting ambao Simba walishinda mabao 3-1 na mchezo wa jana Jumapili.

Akizungumza na gazeti la  Championi Jumatatu, kocha Pablo alisema: β€œTuna kikosi kipana na wachezaji wenye ubora wa kutosha, imani yangu ni kwamba kila mchezaji aliye ndani ya klabu hii hayupo hapa kimakosa bali anapaswa kuisaidia klabu hii.

β€œHivyo nimekaa na wachezaji wote na kuwaambia kuwa nataka kuona wanajituma mazoezini na kila wanapopata nafasi ya kucheza kwa kuwa kila mchezaji atapewa nafasi ya kucheza na kuonyesha alichonacho.”

SOMA NA HII  BAADA YA YACOUBA KUUMIA...NABI AAMUA LIWALO NA LIWE YANGA...AFUMUA KIKOSI KIZIMA CHA KWANZA...