Home CAF KUELEKEA MKUTANO MKUU WA CAF TANZANIA….RAIS SAMIA KUZINDUA ‘SHOW’….RAIS KENYATTA KUIBEBA SUPER...

KUELEKEA MKUTANO MKUU WA CAF TANZANIA….RAIS SAMIA KUZINDUA ‘SHOW’….RAIS KENYATTA KUIBEBA SUPER LEAGUE…


Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa wa 44 wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) utakaofanyika Jumatano Agosti 10 katika ukumbi wa mikutano wa AICC, Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari, Rais wa Shirikisho la soka Tanzania Wallace Karia amesema mkutano huo utajumuisha jumla ya wageni 400 wakiwemo wajumbe halali 156 kutoka nchi 52 wanachama wa CAF.

“Nchi wananchama 54 lakini Kenya na Zimbabwe wameondolewa kwenye mkutano kutokana na Serikali ya nchi hizo kuingilia shughuli za michezo”

Rais Karia alisema katika mkutano huo mbali na wajumbe watakuwepo wageni wengine watakaokuwepo ni pamoja na Rais wa shirikisho la mpira duniani ‘FIFA’ Gianni Infantino ambaye pia amemualika Rais wa shirikisho la soka Qatar kuwakilisha bara la Asia mwingine ni Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika, Patrice Motsepe atakuwepo na wachezaji wa zamani maarufu.

Alisema kuwa ajenda kuu ya mkutano huo ni kupokea taarifa za maendeleo ya mpira wa miguu, taarifa za fedha sambamba na kujadili uanzishwaji wa mashindano ya ‘Afrika Super Cup’

“Tukifanikiwa kukubaliana na kupitisha kwa pamoja mashindano haya yaanze tunatarajia Rais wa Kenya Uhuru Kenyata atatuzindulia rasmi hapa Arusha”. amesema Karia.

Alisema kuwa pia watajadili mashindano mbali mbali ikiwemo klabu bingwa Afrika ‘Afrika championship’ na mashindano ya Shirikisho lengo ikiwa ni kupata fedha za kusaidia kuendesha mashirikisho ya mpira.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa michezo nchini, Yusuph Singo alisema kuwa maandalizi yote kuelekea mkutano huo yamekamilika na wageni wameshaanza kuingia ambapo Rais wa FIFA anatarajiwa kupokelewa jioni katika uwanja wa kimataifa Kilimanjaro KIA.

“Mkutano huu umekuja kutokana na mahusiano na ushirikiano mzuri tuliyonao na Shirikisho letu, hivyo Serikali itaendelea kutoa sapoti kubwa ili michezo nchini iendelee kukua ikiwemo kuboresha viwanja viwe na hadhi ya kimatafa ili tuweze kupata mashindano makubwa”. alisema Singo.

Nae mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela aliwahakikishia wageni wote ulinzi wa kutosha kwa siku zote watakazoishi mkoani humo na mashirikiano huku akiwataka wakazi wa Arusha kuwa wakarimu kuwasaidia wageni watakapohitaji msaada.

SOMA NA HII  GAMONDI AFUNGUKA KILICHOOKOA JAHAZI DHIDI YA AZAM JANA