Home news MUGALU..SAKHO..WAZIDISHA FURAHA MSIMBAZI…UONGOZI WATOA TAMKO RASMI…

MUGALU..SAKHO..WAZIDISHA FURAHA MSIMBAZI…UONGOZI WATOA TAMKO RASMI…

HABARI njema kwa mashabiki wa Simba ni kurejea kwa nyota wawili wa klabu hiyo, Pape Ousmane Sakho na Chris Mugalu ambao tayari wameanza mazoezi baada ya kukosekana kwenye michezo minne iliyopita kutokana na majeraha.

Muga
lu na Sakho walipata majeraha kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji uliopigwa Oktoba Mosi mwaka huu, ambapo kutokana na majeraha hayo mpaka sasa wamekosa michezo minne ya Simba katika mashindano yote.

Simba imeanza kwa kusuasua msimu huu ambao mpaka sasa wanakamata nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi wakiwa wamejikusanyia pointi kumi na mja tu katika michezo mitano waliyocheza mpaka sasa. 

Akizungumza na Championi Jumatano, Mkuu wa Maudhui wa Simba, Ally Shatry alisema: “Baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha, tunatarajia wachezaji Sakho na Chris Mugalu watarejea kikosini baada ya kupona majeraha yao.

“Wachezaji hao wote wawili tayari wameanza programu za mazoezi, na kuendana na mahitaji ya benchi la ufundi tuna matumaini makubwa watakuja kuongeza nguvu katika michezo ijayo.”

SOMA NA HII  BAADA YA DILI LA KUMNG'OA BAJANA KUONEKANA GUMU...SIMBA WATENGA MIL 350 KWA KIFAA HIKI...