Home news PAMOJA NA YANGA KUFANYA VIZURI..NABI AANIKA KILA KITU WANACHOFANYIWA NA GSM..AUTAJA UONGOZI…

PAMOJA NA YANGA KUFANYA VIZURI..NABI AANIKA KILA KITU WANACHOFANYIWA NA GSM..AUTAJA UONGOZI…


BAADA ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam Jumamosi iliyopita kuichapa Ruvu Shooting juzi bao 3-0, kocha wa Yanga Nasredine Nabi amefunguka kuwa ana ushukuru uongozi wa timu hiyo pamoja na wadhamini wao GSM kwa kufanikisha usajili bora ambao unaendelea kutoa matokeo chanya kila siku

Yanga imefanikiwa kufikisha pointi 12 baada ya kuwachakaza Azam FC na Ruvu katika michezo iliyopigwa klwa nyakati tofauti kwenye Dimba la Mkapa hapa Dar es Salaam.

Nabi alisema kuwa anashukuru uongozi mzima wa Yanga na GSM, kwani walimpatia ushirikiano wa kutosha katika kukamilisha usajili wa wachezaji aliokuwa anawahitaji.

“ Tunashukuru kwa haya matokeo tuliopata kwani yatatusaidia kuweza kufikia malengo ya timu ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu.

“Nina ushukuru uongozi mzima wa Yanga pamoja na wadhamini wake GSM kwa sapoti yao kubwa walionipatia katika kipindi cha usajili wamesajili wachezaji ambao nilikuwa nawahitaji pia nina imani kuwa tutafikia malengo yetu kutokana na uwezo mkubwa wa wachezaji wetu,” alisema kocha huyo.

SOMA NA HII  BWANA WEE..KUMBE AL AHLY KAMA SIMBA TU KWENYE DILI LA MIQUISSONE..

1 COMMENT

  1. […] ukiniambia nikutajie wawili kwangu ni Deusdedith Okoyo ambaye (Geita Gold) na Joyce Lomalisa (Yanga) ni miongoni mwa wachezaji bora wanaocheza nawasi […]