Home Uncategorized HIKI NDICHO INAKIKOSA SIMBA NDANI YA LIGI KUU BARA

HIKI NDICHO INAKIKOSA SIMBA NDANI YA LIGI KUU BARA


PASCAL Wawa, beki kisiki ndani ya Klabu ya Simba amesema kuwa ameukumbuka mpira kwa sasa pamoja na mashabiki.

Wawa, raia wa Ivory Coast amekuwa mhimili ndani ya Simba msimu huu ambapo amekuwa akitimiza majukumu yake kwa umakini na kuifanya safu ya Simba ya ulinzi kuwa namba moja kwa safu zilizofungwa mabao machache ikiwa imefungwa mabaoa 15 baada ya kucheza mechi 28.

Akizungumza na Saleh Jembe, Wawa amesema kuwa kuna mambo mengi ambayo ameyakumbuka kwa sasa ikiwa ni pamoja na mpira na mashabiki.

“Nipo nyumbani nikiendelea kufanya mazoezi binafsi ila nimekumbuka mpira ule wa ushindani pamoja na makelele ya mashabiki ni vitu ambavyo kwa sasa ni ngumu kuvipata.

“Unajua wakati tukiwa uwanjani na tunacheza kwa pamoja kuna raha yake ukiwa unaskia mashabiki wanapiga kelele na jadi ya mashabki wa Simba wao ni kawaida yao kupiga makelele ila hamna namna ni lazima tufuate utaratibu afa ni muhimu,” .

Kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imesimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo ni janga la dunia nzima.

SOMA NA HII  MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA