Home Uncategorized MABOSI WA TIMU ZA ENGLAND HOFU TUPU

MABOSI WA TIMU ZA ENGLAND HOFU TUPU


HOFU imeanza kutanda kwa mabosi wa timu mbalimbali zinazoshiriki Ligi Kuu England baada ya jana Serikali ya Ufarasa kufuta shughuli zote za mikusanyiko ikiwa ni pamoja na michezo mpaka mwezi Septemba.

Kauli hiyo iliyotolewa jana na Waziri Mkuu Eduardo Philippe ambaye amesema kuwa hakutakuwa na shughuli za masuala ya michezo mpaka mwezi Septemba kutokana na janga la Virusi vya Corona kumefuta kabisa Ligue 1 na Ligue 2 kuendelea.

Inaelezwa kuwa klabu nyingi zinazoshiriki Ligi Kuu England zimeanza kuwa na mashaka kwamba huenda na Ligi yao ikafutwa ama kulazimishwa kurejea uwanjani hali ikiwa bado shwari.

Tayari Serikali ya Uingereza inaelezwa kuwa ipo kwenye mpango wa kurudisha ligi hiyo ambayo ni pendwa duniani ila haitaruhusu mashabiki kuepusha maambukizi zaidi na kabla ya ligi kuanza wachezaji watakaa hotelini kwa muda wa wiki sita ili kujua hali zao.

Mpaka Ligi Kuu England inasimamishwa vinara walikuwa ni Liverpool ambao wanapewa nafasi kubwa ya kuwa Mabingwa huku ile ya Ligue 1 PSG walikuwa ni vinara mpaka ligi inafutwa.

SOMA NA HII  ZAHERA AWAPA KIBANO ZESCO UNITED - VIDEO