Home news SADIO, SAKHO WARUDISHA TABASAMU MSIMBAZI…IVO MAPUMBA AWANYOOSHEA KIDOLE MAKOCHA SIMBA..

SADIO, SAKHO WARUDISHA TABASAMU MSIMBAZI…IVO MAPUMBA AWANYOOSHEA KIDOLE MAKOCHA SIMBA..


KUREJEA mazoezini kwa nyota wawili Pape Sakho na Sadio Kanoute kutamfanya kocha mkuu wa timu hiyo, Pablo Franco kuwajua mastaa wake katika majukumu yake mapya.

Sadio na Pape walipata majeraha katika michezo ya Ligi Kuu Bara wamerejea kuendelea na majukumu baada ya kusumbuliwa na majeraha hivi karibuni.

Wachezaji wengine Thadeo Lwanga amepewa uangalizi maalum wiki mbili, Sadio Kanote na Pape Sakho waliumia goti huku Chris Mugalu anayesumbuliwa na nyama za paja akiendelea na matibabu.

Hitimana Thiery, kocha msaidizi wa Simba amesema kuwa nyota hao kurejea uwanjani ni faraja kubwa kwake na kocha mkuu Pablo Franco atapata nafasi ya kuwaona. “Ameingia tayari na jioni ya leo (jana) atapata nafasi ya kusalimiana na wachezaji kabla ya kuanza majukumu yake kesho,”alisema.

Mchezaji wa zamani wa Simba, Ivo Mapunda alisema benchi la ufundi la Simba ni zuri hivyo ni wajibu wa wachezaji kufanyia kazi kile ambacho wanafundishwa.

SOMA NA HII  HII HAPA BLACKJACK 2 YA KWENYE MERIDIANBET AMBAYO INATEMA MPUNGA WAKATI WOTE..