Home news SIMBA: PABLO NI ZAIDI YA GOMES …SASA MATOLA APEWA UHURU TOFAUTI...

SIMBA: PABLO NI ZAIDI YA GOMES …SASA MATOLA APEWA UHURU TOFAUTI NA WAKATI WA GOMES…


KOCHA mpya wa Simba, Mhispania Pablo Franco amekuja kwa staili ya tofauti na makocha wengi waliopita baada ya yeye kujichanganya na wachezaji kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.

Pablo alionyesha tofauti hiyo baada ya juzi Jumatatu kwenye mazoezi ya jioni kufika uwanjani akiwa ndani ya gari la wachezaji kitu ambacho huwa hakifanyiki kwa makocha wengine.

Siku yake ya kwanza Jumamosi iliyopita kwenye mechi yao ya kirafiki kocha huyo alikuja na gari lake aina ya Crown Athlete lakini baada ya hapo ni kama ameacha kwenda nalo mazoezini.

Wakati Simba ipo chini ya Kocha Didier Gomes alikuwa haongozani na wachezaji wake pindi anapokwenda mazoezini, kwa sababu alikuwa anatokea hotelini anapoishi moja kwa moja hadi mazoezini.

Hata hivyo, tofauti na Pablo huenda kambini na kuacha gari lake kisha kuungana na wachezaji kwenye basi na kwenda nao mazoezini.

Tofauti nyingine ya Pablo kwa Gomes ni anapokuwa mazoezini na amekuwa akiwa karibu na mpira akifuatilia kwa makini kila hatua.

Kocha huyo huonyesha midadi mikubwa ya kuelekeza wachezaji wake tofauti na Gomes aliyezoeleka kusimama eneo moja.

Pablo ameanza kutengeneza lugha moja upande wa benchi la ufundi kwa kuonyesha kukubali kile anachoelekezwa na wenzake na lengo kubwa likiwa ni kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri.

Kwa namna ambavyo imeshuhudiwa kwenye mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Cambiasso, makocha wote watatu Pablo Franco, Thiery Hitimana na Seleman Matola wapo na morali moja baada ya kila mmoja kutoa ushauri.

Awali wakati wa Didier Gomes baada ya kuja Hitimana ilikuwa ni nadra sana kumuona Matola akinyanyuka kumuelekeza kitu Gomes badala yake aliyekuwa anafanya hivyo ni Hitimana.

Kwa sasa makocha wote wanasimama kwa pamoja na kushauriana na Pablo na kocha huyo anaonyesha wazi kukubaliana nao hali ambayo inazidi kuongeza morali katika benchi lao la ufundi.

Pia ujio wa Pablo wakati wachezaji wengine wakiwa kwenye majukumu yao ya timu zao za Taifa basi upande wa wachezaji ambao wamebaki na kocha huyo mazoezini wanakamua balaa kujaribu kumshawishi kocha waweze kuingia kwenye kikosi chake.

SOMA NA HII  MATOLA:- KWA HALII....MHHH UBINGWA UTAKUWA MGUMU SIMBA....

Pablo ameonyesha kuwa ni kocha ambaye anataka kutumia mbinu zote pindi anapotaka kushambulia uwanjani huku akiwataka mawinga wake kuwa wepesi kupeleka mashambulizi na kupiga krosi ambazo haziendi sana juu na viungo wawe wepesi kupiga pasi zenye macho na zinazoingia moja kwa moja eneo la kati ili washambuliaji wake wafunge.

KIBU, KAGERE WAPEWA KAZI MAALUMU

Kocha huyo alionekana kuweka nguvu zaidi pia upande wa washambuliaji kuhakikisha wanapata mabao mengi kwenye mchezo wao wa leo dhidi ya Ruvu Shooting.

Kocha huyo alikuwa mkali muda wote kwa washambuliaji wake pindi wanapokuwa wanapoteza umakini wanapofika golini na alikuwa anatembea na namna ambavyo mpira unaenda mpaka mwisho.

Kibu Denis kuna muda alikosea kukontroo mpira ndani ya boksi, aliitwa na kuonyeshwa namna anavyotakiwa kufanya kwa kuwa na utulivu pindi anapokuwa ndani ya boksi.

Kocha huyo pia hata upande wa makipa pia alimwelekeza Beno Kakolanya namna ya kukava krosi baada ya kuchelewa kutoka golini pindi mpira ulipopigwa na Gadiel Michael na Meddie Kagere alifunga bao.