Home news BAADA YA KUTEMWA SIMBA…GOMES NA ADEL ZRANE WAPATA KAZI YA MAMILIONI…

BAADA YA KUTEMWA SIMBA…GOMES NA ADEL ZRANE WAPATA KAZI YA MAMILIONI…

 


Aliyekuwa Kocha wa Simba, Didier Gomes Da Rosa, ametangazwa kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa Ya Mauritania.

Gomes ambaye aliachana na Simba, Oktoba mwaka huu, amewahi kufundisha vilabu vya Al-Ismaili, Al-Marreikh ya Sudan, na Simba ya Tanzania.

Gomes anakwenda kuchukua nafasi ya Mfaransa mwenzake Corentin Da Silva Martins, ambaye alifungashiwa virago baada ya matokeo mabaya katika mechi za kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia Qatar 2022.

Pamoja naye, pia kocha wa zamani wa viungo wa Simba, Adel Zrane naye amepata kazi ya kuwa kocha wa viungo wa timu hiyo iliyopo Kaskazini mwa Afrika.

Didier Gomez ataanza kibarua chake na Mauritania katika Mashindano yanayokuja ya Kombe la “Arab Cup” yatakayofanyika Qatar.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA MIQUISSONE NA SIMBA...'UPDATE' MPYA HIZI HAPA KUTOKA AL AHLY YA MISRI...