Home Azam FC NYOTA WAWILI WA AZAM FC KAZINI NA TIMU YAO YA TAIFA YA...

NYOTA WAWILI WA AZAM FC KAZINI NA TIMU YAO YA TAIFA YA UGANDA


 MATHIAS Kigonya kipa namba moja wa Azam FC pamoja na beki wa kulia Nicholas Wadada wapo ndani ya kikosi cha timu ya taifa ya Uganda ,’ The Crane’.

Leo Jumatano Machi 24 wana kazi ya kusaka ushindi dhidi ya Burkina Faso mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika, ( Afcon).


Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Nelson Mandela, Uganda.

Uganda kwenye hatua za makundi ipo kundi B ikiwa inashika nafasi ya pili baada ya kucheza echi nne imekusanya pointi 7.

Kinara wa kundi hilo ni Burkina Faso mwenye pointi 8 kibindoni.


SOMA NA HII  AZAM FC YAINYOOSHA PAMBA FC IKIWA NA KIKOSI KAZI KAMILI