Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA KIBU DENIS NA SIMBA…KUMBE HUYU NDIO ANAYEVURUGA

KUHUSU ISHU YA KIBU DENIS NA SIMBA…KUMBE HUYU NDIO ANAYEVURUGA

Habari za Simba leo

Pichani ni Carlos Sylvester [Mastermind], Agent wa wachezaji mbalimbali kwenye ligi yetu akiwa na viongozi wa Timu za Simba na Yanga.
Pale Yanga anawasimamia wachezaji wawili, Bakari Nondo

Mwamnyeto na Gift Mauya na Simba ana wachezaji wanne ambao ni Mzamiru Yassin, Kibu Denis, Mohamed Hussein na Hussein Kazi.

Kibu Denis, Mzamiru Yassin na Mwamnyeto mikataba yao inaelekea mwishoni, Carlos anafahamu huu ndio wakati wa kutengeneza pesa kupitia wateja wake.

Katika nyakati hizi ni rahisi sana kusikia Mwamnyeto anataka kwenda Simba na Kibu Denis anataka kwenda Yanga ilimradi tu ‘Mteja’ apate thamani anayoitaka Agent.

Iko hivi… Kwenye kujadili mkataba mpya wa Kibu Denis ni rahisi sana Simba kuulizia uwezekano wa kumpata Nondo na pia Yanga wanapojadili namna ya kuongeza mkataba wa Mauya ni rahisi kuulizia huduma ya Kibu, Zimbwe au Mzamiru. Hapa ndipo tetesi zinapozaliwa na kusambaa.

SOMA NA HII  KIBU AWAINGIZA VITANI SIMBA NA YANGA...MRITHI WA LOMALISA YUPO NJIA PANDA