Home news MAYELE AJIPA KAZI YANGA

MAYELE AJIPA KAZI YANGA


 FISTON Mayele, mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa bado wanahitaji pointi tatu katika mechi ambazo watacheza hivyo mapambano yanaendelea.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi jana iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKU SC katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Mkaoa.

Ni Mayele mwenyewe alipachika bao hilo la ushindi kipindi cha kwanza ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa. 

Mayele amesema:”Bado kazi inaendelea kwa kuwa tuna mechi za kucheza kwenye ligi kikubwa ambacho tunahitaji ni kupata pointi tatu,kazi kubwa tutaifanya.

“Ili tufanikishe malengo ambayo tunayahitaji ni kupambana na kupata ushindi hakuna namna nyingine, “.

Katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara, Mayele ametumia dakika 152 na hajafunga bao kwenye mechi hizo ilikuwa Kagera Sugar 0-1 Yanga na Yanga 1-0 Geita Gold. 

SOMA NA HII  BAADA YA KUACHANA NA SIMBA...WAARABU WAMPA DILI LA 'CHAP CHAP' ZORAN MAKI...MSHAHARA WAKE MPYA BALAA TUPU...