Klabu ya Al Ittihad Alexandria ya ligi kuu nchini Misri, imemtangaza Mserbia Zoran Maki (60) kuwa kocha wao mkuu mpya zikiwa zimepita saa kadhaa kocha huyo kutangazwa kuachana na Simba SC aliojiunga nao mwezi Julai mwaka huu.
Zoran ambaye ni raia wa Serbia amondoka Simba na wasaidizi wake akiwemo kocha wa makipa na kocha wa viungo, amesaini mkataba wa miaka mitatu na atalipwa kiasi cha dola 30,000 kwa mwezi (takribani Tsh milioni 60,) na tayari wanatarajiwa kuwasili klabuni hapo muda wowote kwa kuanza kazi.
Kocha huyo ambaye amewahi kufundisha klabu kubwa kama Wydad Casablanca ya Morocco, sasa anakwenda kwenye changamoto mpya ya Ligi ya Misri ambapo klabu yake hiyo mpya imemliza ligi kuu ya nchi hiyo ikiwa nafasi ya 12 ikiwa na pointi 38.
Mserbia huyo ameshinda ubingwa wa Algeria, ubingwa wa Angola mara mbili, na Angola Super Cup katika utumishi wake wa ukocha.