Home news WAKATI SAKATA LA GSM HALIJATULIA…SIMBA WAIBUKA NA LALAMIKO LINGINE…WADAI KUPATA HASARA YA...

WAKATI SAKATA LA GSM HALIJATULIA…SIMBA WAIBUKA NA LALAMIKO LINGINE…WADAI KUPATA HASARA YA Mil 50 …


Klabu ya Simba SC imelalamikia kanuni ya Ligi Kuu inayotoa nafasi kwa klabu Shiriki kuhamisha mchezo kutoka Uwanja wake wa nyumbani na kuupeleka kwenye viwanja vingine.

Simba SC wamelalakia kanuni hiyo, ambayo tayari imeshazinufaisha klabu za KMC FC na Ruvu Shooting zilizotumia viwanja vya Majimaji-Songea na CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mwenyekiti wa klabu ya Simba SC Multaza Mangungu amesema tayari wameshawasilisha malalamiko yao Bodi ya Ligi ‘TPLB’ ili kupitiwa upya kwa kanuni hiyo, ambayo imekua ikiongeza gharama kwa timu mgeni, inapotakiwa kucheza nje ya Uwanja uliokua umetajwa mwanzoni mwa msimu.

Mangungu amesema: “Hii kanuni imekua tatizo kubwa sana, inaongeza gharama ambazo ni nje ya bajeti ya msimu, Simba ilipata wakati mgumu ilipokua Mwanza tulipotakiwa kwenda kucheza dhidi ya Ruvu Shooting.

“Tukiwa Mwanza ilitulazimu kutumia zaidi ya Milioni 50 kwa ajili ya timu yetu, hizi gharama hazikuwepo kwenye bejeti yetu ambayo ilipangwa kutokana na ratiba ya Ligi iliyotolewa kwa msimu huu.”

“Tunahitaji klabu itakayohamisha mchezo kutoka kwenye kituo chake kwenda mkoa mwingine, ikubali kuchangia gharama ambazo zitazidi, hilo ndilo tumelipendekeza kwenye malalamiko yetu.

Hata hiyo Simba SC italazimika kusafiri hadi mkoani Tabora kucheza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya KMC FC ambayo imehamisha mchezo huo kutoka Uwanja wa Uhuru Dar es salaam.

Mchezo huo utachezwa Desemba 24, Uwanja wa Ali Hassn Mwinyi ambao utatumika kama Uwanja wa nyumbani wa KMC FC.

Hii ni mara ya pili kwa KMC FC kuhamisha mchezo kutoka jijini Dar es salaam, awali walifanya hivyo walipocheza dhidi ya Young Africans Mjini Songea mkoani Ruvuma kwenye Uwanja wa Majimaji.

SOMA NA HII  BAADA YA KUMUONA SAKHO..KOCHA WA ZAMANI WA SIMBA SVEN AGUNA KISHA AFUNGUKA HAYA